MWONGOZO
WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA
NA MAYAI.
Kabla
hatujaelezana kwa undani kabisa ufugaji wa kuku wa mayai na nyama nataka nikupe
ushauri wa kiujasiriamali unaweza kuanza kwa kununua vifaranga 300 vya kuku wa
mayai kwa mfano kila kifaranga sh 1000 hadi 1500. Kazi yako ni kuvilisha pumba
na vyakula vingine vya kitaalamu. Baada ya miezi mine hadi mitano vinaanza
kutaga. Kila kuku anataga mayai mawili kwa siku kama watalishwa vizuri na
kuwawekea mwanga wa kutosha. Asubuhi moja jioni moja . Sawana mayai 600 kwa
siku kila yai tuseme uuze kwa sh 150 tu( bei ya jumla) kwa siku una sh 90,000.
Kwa wiki kama sh 540,000 mwezi sh 2,160,000 vipi ukiwa na kuku 500, 7000 au
1000?
Kadhalika
kuku wa nyama. Unanunua kifaranga kwa sh 1500 unakikuza kwa wiki tano (kama
siku 35) na kukiuza elfu tano hadi saba.
Sasa
tuanze somo letu rasmi la ufugaji wenyewe.
Ili
kupata mafanikio ya faida katika ufugaji wa kuku wa nyama, mfugaji inakubidi
kufuata taratibu zilizomo katika mwomgozo huu.
Matayarisho ya banda.
Tayarisha
banda mapema kabla vifaranga havijawasili na liwe na sifa kuu zifuatazo:-
· Liwe na sakafu inayosafishika.
· Liwe na madirisha makubwa ya kutosha.
· Ukuta imara na unaosafishika.
· Paa
imara na lisilovuja.
Usafi
wa banda kabla ya kuingiza vifaranga :-
Banda
na vifaa vyote vitakavyotumika visafishwe kwa makini kwa kutumia maji na baadae
dawa (disinfectant).
Ondoa
mabaki yote ya lita na uchafu wote na kutupa mbali na banda kiasi cha km 1.5.
· Safisha ndani na nje ya banda kwa maji
safi.
· Piga dawa (disinfectant) ndani na nje
ya banda lako.
· Paka chokaa kuta na sakafu nje na ndani
ya banda.
· Weka
matandiko (litter) safi na isyo na vumbi juu ya sakafu safi.
Aina
za litter:-
· Maganda ya mpunga.
· Randa za mbao.
· Maganda ya karanga.
· Magunzi
ya mahindi n.k
AFYA YA KUKU NA USAFI BANDANI.
Ili
kupunguza maambukizo bandani/shambani fanya yafuatayo:-
· Chanja chajo mbali mbali kuzuia
magonjwa, mtafute mtalamu kwa msaada zaidi.
· Peleka kuku mgonjwa au aliyekufa mara
moja kwenye klinik ya mifugo ili kujua tatizo.
· Zuia wageni na wasiohusika kuingia
katika banda/shamba lako, na muhudumu awe na sare/nguo maalum kwa ajili ya
shamba kwa ajili ya shamba hilo.
· Iwapo kuku wataumwa ninakushauri umuone
mganga wa mifugo mara moja . Tafadhali usije kutibu kuku bila kujua tatizo au
maelezo ya mganga wa mifugo.
· Hakikisha
wakati wa kulea vifaranga au kuku wakubwa lita inadumu ikiwa kavu mara
inapotolewa ibadilishwe kwani ni rahisi kupata magonjwa.
UTUNZAJI WA KUKU WA NYAMA.
Utunzaji
wa kuku wa nyama huchukua wastani wa wiki 5-6 ili waive, hii imegawanyika katika
vipindi vikubwa viwili:-
· Kwanza kulea wachanga.
· Pili
kulea kuku wa nyama wenyewe.
Kuna
njia mbali mbali za kulea vifaranga, na vile vile aina ya sehemu za kulelea
vifaranga (brooder) na njia na aina za brooder inategemea, uzoefu wa kulea
vifaranga wa mwenyewe na upatikanaji wa vifaa.
Katika
muongozo huu nitaelezea njia maarufu ambayo inatumiwa na wateja wetu wengi na
vifaa vinavyotumika vinavyotumika vinapatikana kirahisi. Njia hii ni ya brooder
ndani ya chumba.
VIFAA MUHIMU KATIKA BROODER.
1. T andiko safi, maranda ya mbao au
mapumba ya mpunga (rice husks) na liwe kina cha wastani was m 10.
2. Taa ya chemli au bulb ya umeme, taa 1
inatosha kwa vifaranga 300.
3. Sahani/sinia za plastiki au bati kwa
kulisha.
4. Vyombo maalum vya kunyweshea maji (chick
drinker).
5. Jiko la mkaa, jiko 1 linatosha kwa
vifaranga 300.
UTUNZAJI WA BROODER (SEHEMU YA
KULELEA).
Ingiza
vifaranga vyako vyako katika brooder, hakikisha vyanzo vyako vya joto vinakuwa
mbali na jamvi wastani wa cm 30 -40 kuja juu na hapo tayari umeshaweka maji
yenye dawa na chakula katika vyombo ndani ya brooder.
Nafasi
iwe ya kutosha kiasi cha kufanya vifaranga wapate pa kutorokea hali ya joto
inapokuwa kali, weka wastani wa vifaranga 33-34 kwa mita 1 ya eneo (33-34
birds/ m2 ) mpaka
umri wa siku 14.siku ya 15 na kuendelea tumia nafasi ya kuku 8 kwa mita ya eneo
(8 birds/m2).
JOTO LINALOPENDEKEZA WAKATI WA KULEA
VIFARANGA (BROODER TEMPERATURE).
UMRI KATIKA SIKU
|
JOTO LA BROODER(degrees celicius)
|
Siku 1-3
|
34
|
Siku 4-7
|
34-31
|
Wiki ya 2
|
31-27
|
Wiki ya 3
|
27-23
|
Wiki ya 4
|
23-20
|
Wiki ya 5
|
20
|
Source:
shirika la elimu kibaha(2009)
KUMBUKA .
Joto
sahihi ni muhimu sana kwa ukuaji wa wa pamoja na uongezekaji mzuri kwa ukuaji
mzuri wa uzito.iwapo joto litakuwa kali sana na kama baridi itakuwa kali sana
nguvu ya kuku kula hupungua ambayo hupelekea kuku kudumaa.
· Kama joto ni dogo vifaranga
watatetemeka na kufa.
· Kama
hewa haitoshi vifaranga watapata mafua na baadae kufa kwa kukosa hewa
ULISHAJI WA VIFARANGA KATIKA BROODER.
Katika
siku chache za mwanzo vifaranga wapewe chakula kilichosagwa vizuri kiwekwe
kwenye trei au sinia. Trei 20 zinatosha kwa vifaranga 1000.
Utunzaji
wa vyombo vya vyakula wakati wa kukuza kuku wa nyama:
Siku
ya 21, watoe kuku kwenye brooder na hapo wawekee vyombo maalum vya kulishia
kuku (feeders). Kwa kuepuka chakula kisipotee, vyombo vinynyuliwe kwa kufuata
urefu wa kuku.
Mdomo
wa chombo katika sehemu ya kulia kuku, ulingane na mgongo wa kuku mwenyewe.
UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI.
Kuku
wa mayai hana tofauti sana na wanyama katika hatua nyingi ila hutofautiana
kwenye utunzaji
UTUNZAJI WA KUTUNZA KUKU WA MAYAI.
UMRI WA KUKU (WIKI)
|
UZITO WA KUKU (GMS)
|
CHAKULA (GMS)
|
UTAGAJI (%)
|
1
|
78-80
|
10
|
|
2
|
130-140
|
17
|
|
3
|
200-220
|
23
|
|
4
|
280-310
|
28
|
|
5
|
350-400
|
34
|
|
6
|
420-490
|
37
|
|
7
|
490-580
|
40
|
|
8
|
580-660
|
43
|
|
9
|
660-750
|
46
|
|
10
|
740-840
|
50
|
|
11
|
840-930
|
53
|
|
12
|
900-1010
|
56
|
|
13
|
980-1100
|
59
|
|
14
|
1160-1280
|
68
|
|
15
|
1160-1280
|
68
|
|
16
|
1250-1370
|
73
|
|
17
|
1340-1460
|
85
|
|
18
|
1490
|
85
|
|
WEKA MATAGIO
|
|||
19
|
1600
|
92
|
|
20
|
1710
|
100
|
5
|
21
|
1800
|
105
|
20
|
22
|
1870
|
110
|
48
|
23
|
1890
|
114
|
72
|
24
|
1990
|
116
|
84
|
25
|
1960
|
19-130
|
91
|
80
|
UNAWEZA KUWAUZA NA KUWAWEKA WENGINE
|
NUHU YAHYA SALEH O767565039, 0786 565039, 0713 565039
email nuhusaleh33@gmail.com, nuhusaleh33@yahoo.com
Reviewed by Nuhu Saleh
on
12:48:00 AM
Rating:
No comments