MAGONJWA YA KUKU
MAGONJWA YA KUKU
1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili
· Kuhalisha choo cha
kijani na njano
· Kukohoa na kupumua
kwa shida
· Kupinda shingo kwa
nyuma
· Kuficha kichwa
katikati ya miguu
· Kukosa hamu ya kula
na kunywa
· Idadi kubwa ya vifo
hadi 90%
Kinga
· Chanjo (New Castle
vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
· Epuka kuingiza kuku
wageni
· Choma au fukie
mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
· Zingatia usafi wa
mazingira
NDUIYA KUKU/ FOWL POX
Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili
· Vidonda vyenye
utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
· Kukosa hamu ya kula
· Vifo vingi
Kinga
· Chanja vifaranga wanapofikia
mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
· Epuka kuingiza kuku
wageni
· Zingatia usafi wa
mazingira
HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID
· Kuharisha kinyesi
cha kijani na nyeupe
· Kuku hukosa hamu ya
kula
· Kuku hukonda
· Vifo hutokea kidogo
kidogo kwa muda mrefu
· Kinyeshi
hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
· Usafi
· Fukia mizoga
· Usiingize kuku
wageni
· Chinja kuku wote
mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6
MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa
Dalili
· Kuvimba uso
· Kamasizilizochanganyikana
na usaha unaonuka
· Macho huvimba na
kutoa machozi na pengine upofu
· Hukosa hamu ya kula
· Mbawa huchafuka na
kutoa harufu mbaya
Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
· Kuharisha damu
· Manyoya husimama
· Hulala na kukosa
hamu ya kula
MINYOO
Dalili
· Kunya minyoo
· Hukosa hamu ya kula
· Hukonda au kudumaa
· Wakati mwingine
hukohoa
Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili
· Kujikuna na
kujikung'uta
· Manyoya kuwa hafifu
· Rangi ya upanga
kuwa hafifu
· Ngozi kuwa nene,
ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga
Kuzuia
· Ziba mipasuko
sakafuni na kwenye kuta za banda
· Fagia banda mara
mbili kwa wiki
· Nyunyiza majivu au
chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
· Choma masalia ya
mayai yaliyoanguliwa
· Nyunyiza dawa
kwenye viota
· Weka maranda,
majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
· Fuata kanuni za
chanjo
· Tenga kuku wagonjwa
wakae mbali na kuku wazima
UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili
· Kuku hupungua damu,
uzito na kudumaa
· Mifupa huwa laini
na kutokuwa imara
· Hutaga mayai yenye
gamba laini na madogo
· Huwa na manyoya
dhaifu
NUHU YAHYA SALEH O767565039, 0786 565039, 0713 565039
email nuhusaleh33@gmail.com, nuhusaleh33@yahoo.com
MAGONJWA YA KUKU
Reviewed by Nuhu Saleh
on
12:40:00 AM
Rating:
No comments