UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI - 1

UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI - 1

Wiki hii tutajifunza jinsi ya kufuga kuku wa Nyama na mayai.

Lakini kabla hatujaingia kiundani zaidi jinsi ya ufugaji, kwanza tujifunze vitu muhimu ikiwemo chanjo n.k
SIKU YA 1 – 5: Wape GLUCOSE na mchanganyiko mmoja wapo kati ya hii ifuatayo :
1. NEOXYVITAL au OTC PLUS na TYPHOPRIM au TRIMAZIN. FLUBAN na VITAMIN kama vile BROILER BOOST au AMINOVIT au SUPERVIT BROILER au VITALYTE.

CHAKULA : Weka VIGOSTART ambayo ina RIDOCOX kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi ya nne ili kuzuia COCCIDIOSIS. Baada ya kuacha endelea kutumia
RIDOCOX 200g/tani kwa kuzuia COCCIDIOSIS hadi wiki 1 kabla ya kuuza kwa wale wa
Nyama na wanapoanza kutaga kwa wale wa mayai.

SIKU YA 6 : VITAMIN (VITASTRESS).
SIKU YA 7: Chanjo ya NEW CASTLE masaa mawili tu weka maji ya VITAMIN (VITASTRESS) mara baada ya kutoa maji ya chanjo.
WIKI YA 2: Chanjo ya GUMBORO masaa mawili tu halafu endelea na maji ya VITAMIN (VITA-
STRESS).
WIKI YA 3: DOXYCOL au CTC 20% au ANFLOX GOLD au FLUBAN na AMPROLIUM, VITALYTE au VITASTRESS, MOLASSES kwa siku 5 – 7.
WIKI YA 4: Hakikisha kuku wa Nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya VITAMIN (VITASTRESS/
BROILER BOOST/ SUPERVIT BROILER).
WIKI YA 5: Hakikisha kuku wanakuwa katika dozi ndogo ya VITAMIN (VITASTRESS/VITALYTE/ BROILER BOOST/SUPERVIT BROILER).
WIKI YA 6: Wape kuku wa Nyama maji ya VITAMIN asubuhi na matupu jioni.
WIKI YA 8: Wape kuku wa mayai CHANJO YA NDUI dawa ya minyoo (PIPERAZINE au LEVIWORM) Na VITAMIN (SUPER LAYERS). Walishe GROWERS MASH
Hadi miezi mitatu na nusu , tumia LAYERS MASH wakifika miezi mine kamili, pia
Hakikisha wanapata chakula chenye RIDOCOX hadi wanapoanza kutaga pia wape
Majani.
WIKI YA 12: CHANJO YA NEW CASTLE (Rudia kila baada ya miezi mitatu). Masaa mawili kasha
Wape maji ya VITAMIN.
WIKI YA 16: Kata midomo kisha wape NEOXYVITAL kwa siku 3 -5. Andaa viota.
WIKI YA 48: wape VIRUTUBISHO vyenye kuongeza uwingi wa mayai kama vile G.L.P (Kilo 1 kwa
Kilo 50 za chakula wiki ya kwanza na nusu kilo kwa wiki zinazofuata) na VITAMIN.
WIKI YA 52: Chagua kuku wasio na dalili za kutaga kabisa,wenye maradhi sugu na wenye tabia
Zisizofaa (VICES) wauze ili kupunguza gharama.
WIKI YA 72: Tumia V-RID kusafisha mabanda ili kuua vijidudu pia weka maji ya dawa hii kwenye
Kisafisha miguu (Footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (BIOSECURITY) na
Kwamba vifaranga wanaowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo.
WIKI YA 96: Ondoa kuku wote waliozeeka.

N.B KUKU WA NYAMA TUNAWATOA WATAKAPOFIKA WIKI YA 6
UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI - 1 UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI - 1 Reviewed by Nuhu Saleh on 12:06:00 AM Rating: 5

No comments