KILIMO CHA PILIPILI
(iii) PILIPILI
Pilipili ni kiungo
kikali, hutumiwa kwa kukoleza mchuzi na vyakula mbali mbali. Pilipili
zinaweza kupikwa zikiwa nzima au kukatwakatwa na kutumiwa katika
kachumbari; au kuwekwa kwenye siki na achali, au kusagwa na kutumia unga
wake.
Hili ni zao la nchi za
kitropiki, na hutumiwa sana na wakazi wa Bara Hindi, Mashariki ya Mbali.
Amerika ya Kusini na Afrika ya Tropiki. Pilipili huwekwa katika makundi
makubwa mawili, yaani:
1. Pilipili Hoho (Hot
Pepper)- Hizi ni ndogo ndogo, ndefu, nyembamba, na kali sana. Aina
zinazojulikana zaidi ni Green Chilli, Cherry Pepper, Long Cayenne na
Tabasco.
2. Pilipili Manga (Sweet Pepper)- Hizi zina umbo kubwa, nyama
nying, mviringo na ndefu kidogo, siyo kali. Aina zinazojulikana zaidi ni
Sweet, Neapolitan, Keystone, Giant, Ynlo Wonder na california wonder.
Kupanda: Mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa
majuma manane hadi kumi. Kisha miche hupandikizwa bustani kwa umbali wa
sentimeta 45 kwa 90.
Kuvuna: Umri wa
kuvuna zao hili hutegemea aina ya pilipili na matumizi yake. Aina ambayo
ni kubwa na tamu kwa kawaida huvunwa kabla haijapevuka na kugeuka rangi
yake. Pilipili katika hali hii hutumiwa zaidi kwenye michuzi,
kachumbali na kutiwa kwenye makopo.
Pilipili kali,
ambayo mara nyingi ni ndogo ndogo, kwa kawaida huvunwa baada ya kupevuka
na kuwa nyekundu. Halafu hutumiwa katika mapishi na vyakula mbali
mbali, lakini sehemu kubwa zaidi hukaushwa na kusagwa ili kupata unga
wake.
Magonjwa: Damping- off, Bacteria Spot, Fusarium wilt na
Antracnose, ni miongoni mwa magonjwa yashambuliayo zao hili. Tuseme
magonjwa ya pilipili ni sawa na ya Nyanya. Hivyo njia za kupigana nayo
ni sawa.
Wadudu: Wadudu ambao hushambulia zao hi wengi, lakini walio wabaya
zaidi ni Aphids, Cut worm, Flea beetle, Pepper weevil na Pepper Maggot.
Kinga: Parathion 1% au Chlrdane 5%. Dawa itumiwe mara wadudu watokeapo na kurudiwa kila baada ya siku 7.
KILIMO CHA PILIPILI
Reviewed by darasa uchumi
on
3:23:00 AM
Rating:
No comments